Baba Avunja Nyumba Zake Mbili Watoto wake Wasikae

Mzee Iddi Maganga anaemiliki nyumba eneo la Ngarenaro, Arusha amezua gumzo baada ya kuamua kuvunja Nyumba zake mbili kwa madai kuwa watoto wake wanataka kumuua ili waweze kuchukua nyumba aliyoijenga.

Akizungumza na Ayo TV mzee Maganga amesema hivi karibuni zilienea taarifa za kua watu wasiojulikana walivunja nyumba hiyo lakini ni yeye ambaye amewaagiza watu hao wavunje nyumba hiyo ambayo watoto wake walikua wakiishi na kuongeza kua ataiuza muda wowote kuanzia hivi sasa.

Mzee huyo kwa sasa anaishi kwa mtoto wake wa kike kutokana na kipindi cha nyuma kufungiwa kwenye nyumba kwa zaidi ya wiki moja bila kupatiwa chakula, hapa kuelezea mkasa ulivokua.

“Ile nyumba ni ya kwangu Mimi, nimejenga mimi na mke wangu na mke wangu yuko Akhera sasa, kabla mkewangu hajafa, tulikua tunakaa pale, alipokufa ndipo akaja mtoto wangu Abdallah akanifungia ndani nimekaa wiki nzima nakula kinyesi,” alisema Mzee Maganga.

Mzee huyo anasema alikaa ndani wiki nzima mpaka mtu aliyemtaja kuwa ni Mama Masawe alipompigia simu mtoto wake wa kike kumjulisha kuwa hamuoni mzee huyo akienda kuchukua chakula ndipo mtoto wake akaenda na mumewe.

“Walivunja kitasa, wakanitoa na kunipeleka hospitali kupata matibabu na nilipotolewa nikaenda nyumbani kwake,” alifafanua mzee Maganga

Anansema, baada ya muda kupita akaenda kutazama nyumba yake na kumkuta Abdallah anaishi humo na akamkataza asiingie ndani.

“Tulikwaruzana na Abdallah, akaenda kunishitaki na shahidi yake akawa ni dada yake ambaye ni mtoto wangu wa mwisho, wakashindwa hilo jambo hapo nikaona kumbe hawa watu ni wabaya kwangu mimi nikaanza kufanya mipango ya kuuza hii nyumba,” alisema mzee Maganga.

Mzee huyo mwenye jumla ya waatoto sita amesema amewalipa watu kubomoa nyumba hiyo hiyo halafu amuuzie mtu atakayetaka.

Zaidi tazama video hapa chini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *