Harmonize na Kajala Gumzo mtandaoni

Msanii wa Bongofleva na mpenzi wake Kajala Masanja wameendelea kuwa gumzo mtandaoni kutokana na mahaba moto moto kufuatia wawili hao kurudiana.

Wawili hao wamekua wakishea video na picha wakiwa pamoja jambo na kuwafanya mashabiki wao kutoa ya moyoni juu ya mahusiano hayo.

Wanaowachukia nao hawako nyuma, wapo walioonyeshwa kusikitishwa na mahusiano yao kitokana na mikasa waliyopitia wawili hao kabla ya kuachana mara ya kwanza sababu ikitajwa Harmonize kumtongoza mtoto wa Kajala ajulikanae kama Paula.

Licha ya Maneno hayo toka kwa Mashabiki, Harmonize aliona ni bora kufanya anachokiona sahihi kwa moyo wake kwa  kumuomba Kajala msamaha na hatimae kusamehewa na wawili hao kurudi katika mahaba mazito.

Cheki maoni ya wadau hapa chini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *