Baba na Mwana Wahukumiwa Kunyongwa hadi Kufa Mara

Egypt Sentences 22 Militants to Death by Hanging

Matinde Keranganyi (Baba) na Mwita Matinde (Mtoto) wakazi wa Kijiji cha Genkuru wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya mauaji

Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Musoma kupitia Mahakama ya Wilaya Tarime Mkoani Mara, baada ya kushtakiwa kwa kumpiga mawe, kumkata mapanga na kumchoma mkuki Chacha Nyamhaga katika ugomvi wa kugombea ardhi, Mei 25, 2019.

Hukumu hiyo ilisomwa na Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, Frank Moshi.

Awali, Mwanasheria wa Serikali, Yese Temba, alidai kuwa washtakiwa Mei 25, 2019 kwa makusudi wakiwa na silaha za jadi walimvamia Nyamhanga akiwa shambani kwake kumshambulia kwa kumpiga mawe na kuanguka chini na kisha kumchoma mkuki na kumkata mapanga kichwani hali iliyosababisha kifo chake.

Chanzo cha mauaji hayo kimedaiwa kuwa ni mgogoro wa ardhi kati ya marehemu na washtakiwa hao.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na Mwanasheria wa Serikali Temba ulileta mashahidi saba vikiwamo vielelezo na PF3, mganga aliyefanya uchunguzi wa mwili wa marehemu na upande wa utetezi ulileta mashahidi wanne.

Msajili wa Mhakama Kuu, Moshi alisema Mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka bila kuwapo shaka lolote.

Chanzo: Nipashe/  Jamii Forum

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *