Juma Lokole Amtolea Povu Kajala kisa Harmonize

Kupitia Kipindi cha Mashamsham cha wasafi FM mtangazaji Dida Shaibu alimwambia Juma Lokole kuwa kwa sasa amepoteza nuru na amekua mpole kutokana na tetesi za msanii Kajala Masanja na Harmonize kurudiana kwani Lokole amekua akionyesha wazi kutopendezwa na mahusiano ya wawili hao.

Akijibu shutuma hizo toka kwa Mtangazaji mwenzie Juma Lokole na alisema kuwa yeye kinachomuumiza ni yale yaliyotokea na uzalilishaji uliofanyika baina ya wasanii hao.

Amesema, Kajala Amerudi kwa Harmonize sababu ya Njaa na kuongeza kuwa wote wawili wanapenda kiki.

                     Mtangazaji Juma Lokole

Amesema kuwa, mwanaume yuko pale ili mambo yake yaende na hivyo kwa kuwa waliachana kwa kubwa basi watu watarajie kubwa zaidi ya lililotokea awali kutokea.

Lokole amemshauri kajala azingatie kazi yake ya uigizaji wa Tamthiliya na asimame katika msimamo wake jambo ambalo lingemfanya hata Ex wake amuone bora zaidi.

“Kwa matatizo aliyopitia huko nyuma, asingerudi, kaenda kujichoresha. Linalokuja mbele, mimi siombi heri.” Alisema Lokole.

Kuna tetesi za chini chini zinazoendelea katika mitandao ya kijamii kwamba Kajala na harmonize wamerudisha mapenzi yao baada ya kuachana kwa muda sasa.

                                                               Kajala Masanja n a Binti yake Paula

Kilichosemekana kuwaachanisha wawili hao ni tetesi ya kuwa msanii Harmonize alikuwa akimtaka kimapenzi mtoto wa Kajala ajulikanaye kama paula.

Baada ya kuachana na Harmonize aliingia kwenye mahusiano mengine na kasha kumwagana na mtu huyo na baadae kuamua kurudi kwa Kajala kwa kumuomba Msamaha hadharani bila kificho kwa yale aliyokosea.

Mashabiki wamekua na maoni tofauti huku wengine wakiponda suala la wawili hao kurudiana na wengine wakisema kua mapenzi si ya kuingilia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *