Israel Yakataa Silaha Zake Kuuzwa Ukraine

Israel haitairuhusu Ujerumani kuiuzia Ukraine makombora ya kukinga mizinga ya Spike, kulingana na ripoti ya kituo cha Marekani cha Axios siku ya Jumatano.

Kombora hilo linatengenezwa Ujerumani chini ya leseni ya Israel, na Tel Aviv inabidi waidhinishe uuzwaji  wake. Markenai ilimwomba afisa mkuu wa Wizara ya Ulinzi ya Israeli kuidhinishwa wakati wa ziara yake huko Washington mapema mwezi huu, lakini alikataliwa.

Israel ina wasiwasi kuwa wanajeshi wa Urusi wanaweza kuuawa kwa silaha zilizotengenezwa na Israel, jambo ambalo litapelekea Moscow kudhuru usalama wa Tel Aviv nchini Syria, afisa mmoja mkuu wa Israel ambaye hakujulikana jina lake aliiambia Axios.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *