Wananchi watoa ya moyoni Makonda kutaka kuangamizwa

Wadau mbali mbali wametoa yao ya Moyoni kufuatia aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul makonda kufunguka kuhusu watu kutaka kuangamiza maisha yake.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram leo Jumatatu April 11 Makonda aliandika kuwa anafahamu kuna mkakati unaoratibiwa na Makundi matano kuangamiza maisha yake huku akiyataja makundi hayo kuwa ni Wauza Madawa ya Kulevya, Wanufaika na madawa ya kulevya.

Wengine amewataja kuwa ni Mashoga, wanaotaka kulipa kisasi kwa wasaidizi wa Magufuli  na kundi linguine ambalo hajaliweka wazi na kubainisha kuwa anafahamu mbinu zilizoadaliwa kumuuwa na kutengeneza mashahidi wa uongo ili apewe kesi.

Madai hayo ya Makonda yamezua gumzo na kupelekea wadau mbali mbali kufunguka. Soma hapa chini upate kujua zaidi;

Nafahamu kuna mkakati unaoratibiwa na Makundi 5 kuangamiza maisha yangu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *