Rais Samia afanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Machi 31,2022 amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri ambapo George Simbachawene, Waziri wa Katiba na Sheria amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera na Uratibu.

Naye Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Maliasili na Utalii amehamishiwa Wizara ya Katiba na Sheria na Balozi Dkt. Pindi Chana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Sera na Uratibu) amehamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuwa Waziri wa wizara hiyo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *