Urusi Yasema Hakuna cha Gesi ya Bure Ulaya

Msemaji wa Kremlin, amesema kuwa bado Urusi bado haijafanya uamuzi wa mwisho wa jinsi ya kujibu mapigo kwa nchi za Ulaya kama zikikataa kulipia mauzo ya gesi ya Urusi kwa hela yake, lakini akatoa onyo kuwa Urusi haitosambaza mafuta kwa bara hilo bure.

Onyo la Kremlin linakuja baada ya mataifa ya G7 kukataa matakwa ya Urusi kwamba nchi “zisizo rafiki” zilipe mafuta na gesi ya Urusi kwa rubles,sio euro.

“Hatutasambaza gesi bure, hii ni wazi,” Peskov alisema. “Haiwezekani na ni jambo la busara kujihusisha na hisani katika hali yetu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *