Biden: Putin ni Mchinjaji

Akiulizwa juu ya maoni yake kuhusu Putin baada ya kukutana na wakimbizi huko Warsaw, Biden alifunguka na kusema namchukulia Putin kama mchinjaji .”

Huu ni mfululizo wa kumwita PutinĀ  majina yakukasirisha ambapo hivi karibuni alimwita ni muhalifu wa kivita na anatakiwa kushitakiwa, kitendo hiki kiliikasrisha Kremlin na kumwita baloz wa Marekani kwa mahojiano.

Rais wa Marekani pia alisema hana uhakika kwamba Urusi imebadilisha mkakati wake katika uvamizi wake wa Ukraine, baada ya Moscow kusema lengo lake sasa ni “kukomboa” kabisa eneo lililojitenga la Donbass mashariki.

“Sina uhakika wameweza,” Biden alisema alipoulizwa na mwandishi wa habari ikiwa Moscow ilikuwa imebadilisha mkakati wake.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *