Urusi Yataka Ulaya Kununua Gesi kwa Hela zake

Raisi wa Urusi,Vladmir Putin ameipa wiki moja Benki kuu ya nchi hiyo kuangalia na kutengeneza utaratibu wa matumizi ya pesa za ndani (Rubles) kwa wote wanaonunua gesi ya Urusi.

Urusi itakua inakubali malipo kwa rubles tu kwa nchi wanazoziita “Nchi sisizo rafiki” na hapa wakimaanisha nchi zote zilizoiwekea vikwazo.

Akizingumza  katika kikao kazi cha serikali, alisema kuwa Urusi ina mapngo wa kutotumia sarafu zote za nchi zisizo rafiki katika kufanya malipo. Aliongeza kuwa vikwazo visivyo vya kihalali vilivyowekwa juu ya nchi yake pamoja na kuzuia mali kumewakosesha imani na sarafu zao.

“Nimeamua kutekeleza kwa muda mfupi iwezekanavyo seti ya hatua za kubadilisha malipo – ndio, tuanze na hii – kwa gesi yetu asilia inayotolewa kwa nchi zinazoitwa zisizo rafiki kwa rubles za Urusi, ambayo ni kuacha kutumia kila kitu kilichoathiriwa. sarafu za miamala,” rais wa Urusi alisema.

“Haina maana kupeleka  bidhaa zetu kwa EU na Marekani na kulipwa kwa dola au euro,” aliongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *