Ukraine yaua Wanajeshi 15,800 wa Urusi

Mkuu wa Majeshi wa Ulinzi wa Ukraine amedai kuwa , kuanzia Urusi iivamie hadi sasa imepoteza zaidi ya wanajeshi 15,800, vifaru tanks /  530, helikopta 124, ndege za kivita 108.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa FaceBook amedai kuwa pia meli zaidi ya 4, ndege zisizo na rubani 50, mifumo 280 ya kurusha makombora pia imeharibiwa.

Ameongezea pia bado wanendelea kujaza taarifa zaidi na hazijathibitishwa kutokana na mapigano makali yanayoendelea.

Bongo Leo haijaweza kuthibitisha madai hayo kuwa ni kweli au la.

Mara ya mwisho mwisho Urusi kutoa takwimu zake ilikua tarehe 2 Machi iliposema kuwa wanajeshi 498 walikua wameuwawa hadi muda huo.

https://www.facebook.com/GeneralStaff.ua/posts/279494771030275 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *