Waziri Ummy afunguka mafua makali yanayowakuta watu sasa

Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameliongelea tatizo linaloendelea la watu kukumbwa na mafua makali nchini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumatano Machi 23 , Waziri Ummy amekiri kwamba ni kweli Serikali imepata taarifa za uwepo wa mafua lakini Wizara haiwezi kukurupuka juu ya hilo.

Amesema, wanazo saiti za kukusanya taarifa na kuna timu inafanya ufuatiliaji Dar es Salaam na wanasubiri taarifa.

“Ni kweli tumeziskia hizo taarifa za watoto kuugua mafua, tutaliongea baada ya siku mbili tatu baada ya timu yangu kukamilisha, kuna tetesi tumezipata kwamba Uganda kuna ‘Influenza’, hii sio Covid ni aina Fulani ya mafua” Amesema Waziri Ummy.

Amesema, shida iliyopo, waathiriwa hawajaenda kupima kwa hivyo ni ngumu kujua hiyo ni Influenza ya aina gani.
Amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Maafisa Afya kuhakikisha watu wanaopata Mafua wanachukuliwa Sampuli.

Zaidi, Tazama video hapa chini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *