Waziri Mkuu Feki wa Ukraine Apiga Simu

Waziri wa ulinzi wa Uingereza Ben Wallace ameishutumu Urusi kwa “mipango michafu” na kuomba uchunguzi wa kiulinzi ufanyike kwa kile anachodai kuna mtu alimpigia simu na kujifanya ni Waziri Mkuu wa Ukraine siku ya Alhamis!

Kupitia akaunti yake Twitter aliandika

“Leo jaribio lilifanyika mtu kujifanya waziri mkuu wa Ukraine na kuongea nami. Aliniuliza maswali ya kupotosha na baada ya kumgundua nilikata simu”

Wallace ameishutumu simu hiyo na kuiita mfano wa “Mkakati wa proganda wa urusi, uharibifu na siasa chafu”

Urusi ilituma majeshi yake nchini Ukraine mwezi Februari , ikidai serikali ya Kiev imeshindwa kutimiza makubalaino ya mkataba wa Minsk juu ya ukanda wa Donbass.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *