Mbunge Keisha ashangaa kukosa Mrabaha

Mbunge wa Viti Maalumu Khadija Shaaban Taya maarufu kama Keisha ameshangazwa na kitendo cha kukosa Mirabaha yake licha ya nyimbo zake kuwa zinapigwa sehemu nyingi nchini.

Hayo ameyasema leo Jumanne Februari 8 wakati akichangia mada bungeni ambapo wabunge wameanza kujadili kuhusu mswaada wa sheria mbalimbali wa mwaka 2021.

Licha ya kukosa Mrabaha, Keisha ameipongeza hatua hiyo kwa kusema kwamba mwanzo ni mzuri na kazi nzuri imefanyika.

“Mimi Mrabaha wangu sijapata, nashangaa sana kwa sababu Tanzania nzima inafahamu nyimbo zangu zimekua zikipigwa sehemu nyingi,” Alisema Keisha

“Lakini naamini mwanzo ni mzuri, mmefanya kazi nzuri, tunaamini kabisa mnaenda kufanya mapinduzi ya hizi tuzo na tumeambiwa kabisa hizi tuzo hazitopendelea ” Aliongeza Keisha

Aidha, Keisha, amemshukuru Rais Samia na Serikali yake kwa usikivu wa mambo na kuona namna ya kubadilisha Sheria ziweze kutekelezeka kwa urahisi zaidi.

Januari 28, 2022 kwenye hafla ya uzinduzi wa utoaji wa tuzo za muziki na ugawaji wa mirahaba kwa wasanii iliyofanyika katika  Ukumbi wa kimataifa cha Julius Nyerere. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amesema Wizara hiyo kupitia taasisi ya Hakimiliki na Hakishiriki (COSOTA) itaanza kugawa mirahaba kwa kazi mbalimbali za wasanii zinazotumika kwenye redio kila baada ya miezi sita.

Katika siku hiyo, COSOTA iliwagawia wasanii wa muziki mirabaha yao ambapo Kwaya ya Mtakatifu Cecilia ya Arusha waliongoza kwa kupata hundi ya milioni 8.7 ikifuatiwa na msanii Alikiba ambaye alipokea milioni 7.5 na Rose Muhando ambaye alipata milioni 5.7.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *