DONDOO ZA LEO; Lissu Atua Chato/ Awasema Aliyewahi Kumshitaki Mungu Mahakamani /

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini siku ya leo.

Zinazobamba asubuhi hii ni pamoja na Lissu kutua miguu Chato, Mbowe awsema kina Sumaye na mwisho ni juu ya jamaa aliyemshitaki Mungu, kulikoni? Karibu;

LISSU NA CHATO

ALIYEKUWA mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania, Tundu Lissu amejitosa kwenye mjadala wa kuundwa kwa mkoa mpya wa Chato.

Mjadala huo umetibua hali ya hewa nchini Tanzania, kutokana na mitazamo tofauti, baadhi wakitaka uruhusiwe kuwa mkoa, wengine wakipinga kwa hoja kwamba hauna vigezo.

Katika maoni yake kuhusu mjadala huo, Lissu ameungana na mtaalam wa makazi na Waziri wa zamani, Profesa Anna Tibaijukana ambaye amesema pasi na shaka kuwa Chato haina hadhi ya kuwa mkoa.

Soma zaidi>>>

MBOWE AWASEMA LOWASSA, SUMAYE

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, ametaka wafuasi wa chama hicho waliokimbilia Chama Cha Mapinduzi (CCM), wasidharauliwe.

Mbowe ametoa wito huo  Alhamisi, tarehe 3 Juni 2021, jijini Mwanza, akizungumza na wanachama wa Chadema Kanda ya Victoria.

Miongoni mwa wanachama wa Chadema waliorejea CCM, ni aliyekuwa Mgombea urais wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Edward Lowassa. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye na aliyekuwa Mwenyekiti Chadema Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu.

Soma zaidi>>>

JAMAA ALIYEWAHI KUMSHITAKI MUNGU

Seneta Ernie Chambers wa jimbo la Nebraska, Marekani mwaka 2008 alimshitaki Mungu akiiomba Mahakama itoe zuio la kudumu dhidi ya Mungu kufanya shughuli zake zenye madhara kama mafuriko, matetemeko ya ardhi, vimbunga, tufani na majanga mengine
Inadaiwa katika shauri hilo watu wengi wamekuwa wakijitambulisha kama Mawakala wa Mungu na kufanya mambo mengi maovu lakini hata siku moja Mungu hajajitokeza hadharani kuwakana hivyo wanafanya yote kwa niaba yake na jina lake.
Tukimalizia dondoo hebu tuangalie kidogo nguvu utulivu ya kukaa peke yako  kufikiri

Matatizo makubwa uliyonayo kwenye maisha yako, ni matokeo ya kushindwa kukaa peke yako kwenye eneo tulivu na kufikiria bila ya kuwa na usumbufu wa aina yoyote ile

Ukiwa umekaa karibu na mtu na simu yake ikaita, utaangalia na yako pia. Ukipata dakika chache za kuwa mpweke, haraka sana utakimbilia kuangalia simu yako, kuingia mitandaoni, kufuatilia habari na kadhalika

Asilimia kubwa ya watu wanalala na simu zao, tena zikiwa wazi na hivyo kuruhusu usumbufu hata kama wamelala na wengi kitu cha kwanza wanachofanya wanapoamka ni kuangalia simu zao

Jijengee tabia ya kuwa na muda wa utulivu kwenye kila siku yako, muda ambao unakaa wewe peke yako na mawazo yako, na hakuna usumbufu wowote unaokuwa karibu na wewe katika wakati huu

Mwanzoni utakapokaa tu utaanza kufikiria vitu vingi ambavyo ungeweza kuwa unafanya, mambo mazuri yanayoendelea mtandaoni ambayo yanakupita, lakini usiruhusu hayo yakuondoe kwenye utulivu wako

Anza zoezi hili na utaona jinsi ambavyo maisha yako yabadilika, Msongo utapungua, wasiwasi na mashaka ya kupoteza vitu yataondoka kabisa na utajiona unayaendesha maisha badala ya maisha kukuendesha wewe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *