Dondoo za leo: ATCL yadaiwa Bil. 241 Zanzibar/ Wakina Msigwa Waenda Mahakamani / Mbowe Alaumu Wagombea 2020

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba leo ni pamoja na deni la ATCL Zanzibar, ni la lini? Sugu na Msigwa watinga mahakamani, kulikoni? Na mwisho ni juu ya Mbowe kulia na wagombea 2020, kivipi? Karibu;

AIR TANZANIA NA DENI LA BIL 241 ZENJI

Kaimu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Zanzibar, Abdallah Kombo, jana alisema kuwa Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) linadaiwa Sh.bilioni 241 na Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar ikiwa ni ada ya utuaji na uegeshaji wa ndege za Shirika hilo kwenye Uwanja wa Ndege wa Amani Abeid Karume Zanzibar.

Kombo alibainisha hayo alipojibu swali kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Rahma Kassim Ali, katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kilichofanyika Chukwani, Zanzibar.

Soma zaidi>>>

MSIGWA & SUGU  MAHAKAMANI

WABUNGE wa zamani wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini Tanzania- Chadema, Mchungaji Peter Msigwa na Joseph Mbilinyi maarufu ‘Sugu’ wamewafungulia mashtaka Kamishna wa Magereza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) nchini humo kupinga adhabu zinazotolewa kwa wafugwa magerezani. Anaripoti Nasra Bakari, DMC…(endelea)

Hayo yametolewa jana Jumatano, tarehe 2 Juni 2021, mkoani Dar es Salaam na wanasiasa hao wa upinzani, walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari.

Soma zaidi>>>

MBOWE NA WAGOMBEA 2020

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, amesema baadhi ya Wagombea hawakuwa wakikubalika kwenye maeneo waliyogombea katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Mbowe amesema “Nikiri kuna maeneo mengi tulikuwa na Wagombea sahihi, lakini maeneo kadhaa tulikuwa na Wagombea dhaifu, huo ni ukweli na haupingiki kwasababu Waswahili wanasema Wali wa kushiba unaonekana kwenye sahani”
Ameongeza “Sasa hivi Wanachama wetu ni ambao hawazidi umri wa miaka 45, hii ni dalili nzuri kwamba Upinzani utakuwa imara zaidi lakini tunapambana kuhakikisha kila kitu tunachokifanya kinafanyika kidijitali”

Soma zaidi>>>

Kumalizia dondoo hebu tuangalie jambo hili lililomkera mdau wetu juu ya watu kuwa na tabia ya kuwabusu watoto mdomoni.

Amesema, “Unakuta mtu kaja kutembelea mtoto wako au kamkuta umemshika anamchukua na kuanza kumpiga mabusu ya mdomoni. Huu ni uchafu sana mimi sipendi kabisa tabia hiyo”

Kimaadili tunaona haiko sawa sina hakika kama na wewe ungekipenda kitendo hicho.

Una maoni gani katika jambo hili?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *