Oman ‘kuiwekea Tanzania marufuku ya kusafiri’

Tanzania huenda ikawa miongoni mwa nchi ambazo zitapigwa marufuku ya kusafiri kwenda nchini Oman, ikiwa ni sehemu ya kupambana na maambukizi ya Corona nchini humo.

Vyombo vya habari vya Oman vimeripoti vikimnukuu Waziri wa Afya nchini humo.

Dkt. Ahmed bin Mohammed Al-Saeedi amesema kuwa takwimu zinaonesha kuwa wasafiri wanaotoka Tanzania, asilimia 18 kati yao wanakutwa na maambukizi ya corona. ‘’ambayo ni idadi kubwa sana’’ anasema.

Amesema kuwa kamati inayoshughulikia masuala ya corona inataka kuzuia ndege zinazofanya safari kwenye maeneo yenye maambukizi mengi.

Serikali ya Tanzania haijatoa taarifa mpya za maambukizi ya corona au vifo, mara mwisho ilikua mwezi Aprili mwaka jana.

Msemaji mkuu wa serikali nchini Tanzania Dkt. Hassan Abbas alisema Tanzania inazingatia miongozo yote ya tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona na hata wakati huu ambao dunia inapambana na wimbi la pili la maambukizi ya virusi hivyo.

Chanzo; BBC

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *