Dondoo za leo; Lema akamatwa Kenya/ Kurudishwa leo/ Chama chamtenga

Habari yako mdau wa Opera News, tunatumai u Bukheri wa Afya

Karibu kwenye dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini siku ya leo.

Zinazobamba ni pamoja na Lema kukamatwa Kenya, kurudishwa na mwishio ni juu ya CUF kumtengua Naibu Katibu wake, kulikoni? Karibu;

LEMA AKAMATWA KENYA

Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),

Godbless Lema amekamatwa na Polisi katika kaunti ya Kajiado nchini Kenya baada ya yeye na familia yake kuvuka mpaka wa Namanga.

Maafisa wa Uhamiaji walikatas kugonga muhuri nyaraka zilizowasilishwa na mke wa Lema kwa madai hadi wamuone Lema.

Lema alikwenda, akawaambia hana hati yake ya kusafiria kwa sababu alikuwa hasafiri, bali wanaye walikuwa wanakwenda kutafuta Shule ya Kimataifa.

Maafisa waliruhusu mke na watoto kuvuka mpaka, Lema aliomba kwenda kutafuta fedha za Kenya ili ampe mke wake.

Soma zaidi>>>

KENYA KUMRUDISHA LEMA

Kenya imesema aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema atarudishwa Novemba 9, 2020 baada ya kwenda nchini humo kutafuta hifadhi kwa UNHRC.

 Lema anayeshikiliwa Kituo cha Polisi cha Kajiado amedai maisha yake yapo hatarini.

CUF YAMTENGUA

Chama cha CUF kimetengua uteuzi wa Kaimu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Ali Makame Issa kwa kosa la kujitokeza kuwania Uspika wa Baraza la Wawakilishi bila ridhaa ya chama

CUF iliweka msimamo wa kutotambua matokeo ya Uchaguzi Mkuu kwa Urais, Ubunge, Uwakilishi na Madiwani

Chama hicho kimesema, Ali Makame ni miongoni mwa Wajumbe walioshiriki Vikao vilivyopitisha Maamuzi ya Msimamo wa Chama kuhusu Uchaguzi Mkuu ulioharibiwa, lakini Novemba 7 alijitokeza katika mchakato wa kumpata Spika wa Baraza la Wawakilishi

Chama kimewaomba radhi Watanzania kutokana na ukakasi uliosababishwa na Ali Makame Issa kwa kujitokeza kwake hadharani kugombea nafasi ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar bila ya ruhusa ya Chama

Chanzo; Jamii Forum

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *