Dondoo za leo; Kunani? Tundu Lissu kujikabidhi Ujerumani/ Wauana wakipigania maduara/ Viti maalumu mtihani

Habari yako mdau wa Opera News, tunatumai u Bukheri wa Afya

Karibu kwenye dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini siku ya leo.

Zinazobamba ni pamoja na Lissu kukimbilia Ubalozi wa Ujerumani, wapigana kisa maduara, kulikoni? Na mwisho ni juu ya mtihani wa viti maalumu CHADEMA. Karibu;

TUNDU LISSU AJIWEKA UJERUMANI

ALIYEKUWA mgombea urais wa Chadema, katika uchaguzi mkuu uliyopita nchini Tanzania, Tundu Antipas Lissu, amekimbilia nyumbani kwa balozi wa Ujerumani, jijini Dar es Salaam, “kuomba hifadhi ya maisha yake.”

Taarifa kutoka kwa watu waliokaribu na kiongozi huyo zinasema, Lissu pamoja na baadhi ya wasaidizi wake, wapo nyumbani kwa balozi huyo, kufuatia mwanasiasa huyo, kupokea vitisho lukuki vinavyolenga kuondoa maisha yake.

Lissu na baadhi ya wasaidizi wake, wamekuwa nyumbani kwa balozi wa Ujerumani, nchini Tanzania, tokea Jumatano iliyopita ya tarehe 4 Novemba, 2020.

“Ni kweli kwamba niko nyumbani kwa balozi. Nimekuja kuomba hifadhi, ili kunusuru maisha yangu,” alieleza Lissu na kuongeza, kuondoka nyumbani kwa balozi huyo au kuendelea kuwapo kutategemea, hakikisho la usalama wake.

Soma zaidi>>>

Chanzo; Mwanahalisi

WAGOMBANIA MADUARA

Wachimbaji wadogo nane katika machimbo ya Dhahabu ya Irasanilo, Buhemba, Wilayani Butiama wajeruhiwa kwa silaha za jadi ikiwemo mapanga na visu.
Chanzo cha purukushani hiyo imedaiwa kuwa ni kugombania maduara ya uchimbaji.
Majeruhi wamesema wakiwa wanaendelea na uchimbaji ndani ya shimo, walivamiwa na kundi la watu ambao walianza kuwashambulia.
Mmiliki wa duara hilo, Mwajuma Seif amesema kabla ya tukio, duara hilo lilikuwa na mgogoro.

Chanzo; Jamii Forum

VITI MAALUMU MTIHANI CHADEMA

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania, kinakabiliwa na mtihani mwingine mzito juu ya hatma ya nafazi zake za wabunge wake wa Viti Maalum.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini humo zinasema, wapo baadhi ya viongozi wandamizi wa Chadema wanaounga mkono na kushinikiza chama kikubali kufanya uteuzi wa nafasi, huku kuna wengine wakipinga uteuzi huo.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa wetu, wanaopinga hoja hiyo, wanajiekeleza kuwa, kufanya uteuzi wa wabunge wa viti maalum, ni sawa na kuhalalisha mchakato mzima wa uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatano ya tarehe 28 Oktoba 2020.

Soma zaidi>>>

Chanzo; Mwanahalisi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *