Zitto: Gari Imezunguka Mara tano, gari yetu imetugonga

Kiongozi wa chama Cha ACT-Wazalendo , Zitto kabwe ameeleza tukio la ajali waliyopata ilivyokuwa na kusema kuwa aliona gari ikiwa inazunguka kama mara tano.

Akizungumzwa akiwa hospitalini alikolazwa kwa ajili ya Matibabu Zito amesema, walikua kwenye Mkutano ambapo wakaondoka kuwahi mkutano unaofuata.

“Ilikua kama saa nane kasoro hivi. Baada ya Kama nusu saa ndio tukapata ajali. Sikujua chanzo cha ajali mwanzoni, niliona kama mara tano hivi gari inazunguka, bahati nzuri, wote tuliokua kwenye gari tumetoka salama”. Alisema zitto

“Baadae nikawa nimetaarifiwa kuwa, gari yetu ya nyuma, aliyokuwa akiitumia mgombea wetu wa Ubunge Kigoma Kusini ndio iliyotugonga na zote zilikua zinaenda kwa kasi kwa ajili ya kuelekea kweney mkutano unaofuata.”

Zito alifafanua kuwa, sababu ya vumbi, gari zikawa hazionani hivo wakapata ajali lakiniwalipata huduma ya kwanza kutoka kwa watu wa kituo cha afya.

“Baada ya kuenda kituo cha Afya ikaonekana kwamba bega langu la kushoto ndo lenye matatizo, inaonekana kuna mfupa umevunjika lakini haijathibitishwa mpaka nipate X-Ray.”

Amesema, kwa sasa wanaendelea vizuri ila wanaandaliwa usafiri kuenda Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi na uchunguzi wa kina.

Zitto amemshukuru Mwenyezimungu kwani wote waliopata ajali wapo salama na amewashukuru watu wote kwa maombi.

Kama ulipitwa

Zitto kabwe alipata ajali ya gari akiwa njiani akitokea kata ya Kalya kuelekea Lukoma kwenye kampeni katika jimbo la Kigoma Kusini Oktoba 6,2020.

Zitto alikuwa na watu 5 kwenye gari yake na wote wako salama ingawa wamepata majeraha na wanahisi maumivu makali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *