Dondoo za leo; Lissu kiburi aigomea NEC/ Simanzi,vilio vyatawala/ JPM atema siri

Habari yako mdau wa Opera News, tunatumai u Bukheri wa Afya

Karibu kwenye dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini siku ya leo.

Zinazobamba ni pamoja ni pamoja na Lissu kuigomea NEC, Vilio vyatawala msiba wa kiongozi CCM na mwisho ni juu ya JPM kutema siri ya Dodoma ni ipi? Karibu;

LISSU KIBURI AIGOMEA NEC

TUNDU Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokraisa na Maendeleo (Chadema) amesema, leo Jumanne tarehe 29 Septemba 2020 hatokwenda mbele ya Kamati ya Maadili ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Amesema, tume hiyo inapaswa kwanza kuzingatia Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2020.

Lissu amesema hayo leo jioni Jumatatu tarehe 28 Septemba 2020 wakati akihutubia mkutano wa kampeni za urais Jimbo la Serengeti Mkoa wa Mara.

Kauli hiyo ya Lissu inakuja ikiwa ni siku moja imepita tangu, Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Dk. Wilson Mahera kuutangazia umma juu ya tuhuma za uvunjivu wa maadili uliofanywa na Lissu.

SIMANZI,VILIO VYATAWALA

Simanzi na vilio vimetawala kwa ndugu jamaa na marafiki pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi katika kumsindikiza kwenye safari yake ya mwisho  Mwenyekiti wa Senet mkoa wa Iringa Emmanuel Polycup Mlelwa  kijiji kwao Ruhuyo wilayani Ludewa mkoani Njombe.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama hicho, viongozi wa kidini pamoja na viongozi wa serikali ambao kwa pamoja wamelaani vikali kitendo hicho cha mauaji.

Akizungumza katika mazishi hayo mkuu wa mkoa wa Njombe Injinia Marwa Rubilya amesema atahakikisha wale wote waliohusika na kitendo hicho Cha mauaji anachukuliwa hatua Kali ya kisheria.

Aidha kwa upande wa mmoja wa ndugu wa marehemu Silvanus Msigwa amesema mnamo September 20 mwaka huu walikuwa wanamtafuta ndugu yao kwenye simu lakini walikuwa hawampati wakati si kawaida yake ndipo wakatoa taarifa polisi ili kuweza kupata msaada.

JPM ATEMA SIRI

MGOMBEA wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Magufuli amewambia wapiga kura wake kuwa anasiri kubwa na nzito ndani ya moyo wake juu ya jiji la Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine ameutaja uamuzi wake wa kuhamia Dodoma kuwa ni kutokana na upendo mkubwa alionao kwa watani zake Wagogo.

Mapema jana Septemba, 28, akiwahutubia wakazi wa Chipogolo (Dodoma) mgombea huyo wa CCM alisema kuwa anatamani kuona jiji la Dodoma linazidi kustawi maradufu zaidi ya jiji lolote nchini, huku akitaja miundo mbinu mbalimbali ambayo inajengwa katika jiji hilo kama kichocheo cha kulikuza jiji hilo dhidi ya majiji mengine.

“Tunataka Dodoma tuibadilishe hiyo ndiyo siri iliyomo moyoni mwangu, nataka Dodoma ndilo liwe jiji kubwa kuliko majiji yote katika nchi ya Tanzania, tumejipanga vizuri mno na ndiyo maana hata ring road ya kilometa 110 yenye njia nne tunaanza kuzijenga huku” amesema Dkt John Magufuli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *