Dondoo za leo; Lissu matatani/ Mwili wake wapatikana /Wafungiwa

Habari yako mdau wa Opera News, tunatumai u Bukheri wa Afya

Karibu kwenye dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini siku ya leo.

Zinazobamba ni pamoja na Lissu matatani, mwili wa kada ya CCM wapatikana na mwisho ni juu ya uwanja wa Jamhuri kufungiwa. Karibu;

LISSU MATATANI

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania imemuita Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema katika kikao cha kamati ya kitaifa ya maadili tarehe 29 Septemba 2020.

NEC imesema, Lissu anapaswa kufika siku hiyo ili kutoa maelezo na ushahidi wa kile alichokisema kuwa Dk. John Pombe Magufuli, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) alikutana na wasimamizi wa uchagunzi nzima nchi nzima.

Hayo yamesemwa leo Jumapili tarehe 27 Septemba 2020 na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Wilson Mahera alipozungumza na waandishi wa habari jijini Arusha alikokwenda kwa ajili ya kukagua maandalizi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020.

MWILI WA KADA WA CCM WAPATIKANA

Jeshi la Polisi mkoani Njombe limethibitisha kuokotwa kwa mwili wa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa, Emmanuel Polycarp Mlelwa aliyekuwa amepotea katika mazingira ya kutatanisha.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Njombe, Hamisi Issa ameiambia TBC kuwa jeshi la polisi mkoani humo linaendelea na uchunguzi na litaendele kutoa taarifa kuhusiana na tukio hilo.

Mlelwa alikuwa mwenyekiti wa seneti ya wananfunzi wa vyuo na vyuo vikuu wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa na mwili wake umekotwa katika eneo la Kibena Bwawani.

UWANJA WA JAMHURI WAFUNGIWA

MARA baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga, Bodi ya Ligi imepiga marufuku kutumika kwa Uwanja wa Jamhuri uliopo mkoani Morogoro kutumika katika michezo yote ya kimashindano.

Bodi ya Ligi imewataka wahusika wa uwanja huo kufanya marekebisho katika eneo la kuchezea (pitch), vyumba vya kubadilishia nguo na sehemu za kukaa wachezaji wa akiba.

Kiwanja hicho ambacho jana kimechezwa mchezo wa ligi na kushuhudia Yanga ikiibuka na pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0.

Mpaka sasa bodi hiyo imefungia jumla ya viwanja vimne kutumika katika michezo ya kimashindano ambavyo ni Ushirika Moshi, Mabatini Pwani, Highland Estates uliokuwa ukitumiwa na Klabu ya Ihefu uliopo Mbalizi, Mbeya na Uwanja wa Gwambina

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *