Mnyika “Tutashinda Hata Kama Mwenyekiti Wa Tume Akiwa Magufuli”

Image

Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo John Mnyika amesema chama hicho kimejipanga kushinda kwenye uchaguzi mkuu ujao licha ya  kuingia kwenye uchaguzi bila kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi itakayo simamia uchaguzi huo.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa sera mbadala ya vijana Jijini Mwanza Mnyika amesema chama hicho kitashinda kwa nguvu ya umma hata kama mwenyekiti wa tume atakuwa rais wa awamu ya tano Dkt John Magufuli.

“Mahakamani, ila kwa hali ilivyo mpaka sasa tunakwenda kwenye uchaguzi bila tume huru, na mimi ninawaambia tutashinda kwa nguvu ya umma hata Magufuli angekuwa Mwenyekiti wa tume,”amesema Mnyika.

Kwa muda mrefu sasa vyama vya upinzani vimekuwa vikitaka kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba na tayari kuna kampeni kadhaa zilizoanzishwa kwenye mitandao ya kijamii kushinikiza kuwepo kwa tume hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *