Lema Kuchukua Fomu ya ubunge kesho

DailynewsAliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema ameweka wazi kuwa kesho Agosti 18, 2020 ataenda kuchukua fomu ya kugombea ubunge kwenye tume ya uchaguzi ya uchaguzi kwa ajili ya kugombea kwenye uchaguzi ujao.

Lema ambaye ameongoza jimbo hilo kwa takribani miaka 10 amejinasibu kupitia ujumbe aliotuma kwenye mtandao wa twitter  kuwa anataka kuendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo.

“Kesho nitachukua fomu ya kuendelea kuwa Mbunge wa Arusha Mjini.” ameandika Lema.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *