Waziri wa Elimu Kenya atangaza shule kufunguliwa mwakani

Waziri wa Elimu nchini Kenya, Profesa George Magoha, ametangza shule za sekondari na msingi kufunguliwa mwakani.

Waziri Magoha amesema uamuzi huo ni kutokana na athari za ugonjwa wa Corona.

“Shule za sekondari na msingi zitafunguliwa rasmi mwaka 2021 hii ni kutokana na athari za ugonjwa wa Corona,” amesema Waziri Magoha.

Waziri huyo amesema uamuzi huo wa kufungua shule mwaka 2021 ulichochewa na kuongezeka kwa idadi ya visa vya maambukizi ya virusi vya corona nchini.

Magoha pia amedai kuwa wizara hiyo ilitambua kutekeleza sheria ya kukaa mbali na masharti mengine huenda ikawa changamoto katika shule za msingi na sekondari kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi.

“Tuliamua kuahirisha kufunguliwa kwa shule hadi Januari 2021 kwa sababu tuna imani kufikia wakati huo makali yatapoa na idadi kupungua na pia tutakuwa tumejifunza mengi kuhusu virusi hivyo,” amesema Magoha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *