Aina ya Damu Ambayo Ina Hatari Kubwa ya Kuambukizwa Covid19

Blood types and COVID-19 risk confirmed

Imebainika kuwa watu ambao wana damu aina ya A wako katika hatari kubwa zaidi kuambukizwa virusi hatari vya corona, hii ni kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika jarida la  New England Journal of Medicine.

Kulingana na utafiti huo, watu ambao wana damu aina ya O ni vigumu mno kuambukizwa virusi hivyo ukilinganishwa na wale wa A.

Utafiti huo ulifanyiwa sampuli zote za damu ulilenga kubaini uhusiano ambao virusi vya Covid 19 unavyo na kila aina ya sampuli ya damu.

Uchunguzi huo ulifanyiwa takriban waathiriwa 1,610 wa corona waliokuwa katika hali mahututi nchini Uispania, nchi ambayo imepata pigo kubwa tangu kulipuka virusi hivyo duniani.

Watafiti ha walibaini kuwa sampuli za damu za A zina kiwango kikubwa cha 45% kuambukizwa virusi hivyo ikilinganishwa na sampuli zingine.

Intentional about Diversity: Medical researches in Milwaukee ...

Kwa upande mwingine, watu wenye damu aina ya O hawako katika hatari kubwa ya kuambukizwa virusi hivyo kwa 35%.

Licha ya utafiti huo, haijabainika ni kwanini aina ya damu huchangia dhidi ya kinga kuhusiana na virusi vya corona.

Utafiti huo unasubiri kufanyiwa uchunguzi zaidi kabla kutolewa sababu mahususi kuhusu matokeo hayo.

Covid-19 Changed How the World Does Science, Together - The New ...

Aidha, watafiti hao wameeleza kuwa uchunguzi wao utachangia pakubwa katika juhudi za kutafuta chanjo kwa virusi hivyo hatari.

LIcha ya maangamizi ya virusi vya corona, baadhi ya nchi zimeanza kupiga hatua katika kufungua baadhi ya miundo msingi iliyofungwa, Tanzania ikifungua tena shule na uchumi kwa jumla kusonga mbele.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *