Mbunge Lijualikali aanika siri za Chadema, amtaja Lissu

Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali, ambaye alikuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kabla ya kutangaza kuhama hivi karibuni, amejitokeza na kueleza mambo lukuki kuhusu Chama hicho.

Akiongea na waandishi wa habari leo Mei 23, 2020 amesema chama hicho kina matumizi mabaya ya fedha huku akieleza kuwa hata ripoti ya CAG inaeleza juu ya mapungufu hayo.

Mengine ambayo ameeleza Lijualikali ni juu ya matumizi ya fedha ambazo walikatwa ili zitumike kwaajili ya uchaguzi mkuu wa 2020, ambapo ameweka wazi kuwa zaidi ya Sh milioni 400 zilitolewa kwenye akaunti ili kwenda kumtibu Tundu Lissu alipopigwa risasi mwaka 2017.

‘Tumetoa pesa zetu za mfukoni na kukatwa sh laki tano lakini Mwenyekiti Freeman Mbowe yeye ndio ana saini ya akaunti zote hivyo amekuwa akitoa pesa bila hata wengine kuhusishwa”, – Lijualikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *