Heche: Malori yamekwama mpakani siku ya tisa na mizigo inaharibika

Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche, amesema mpaka wa Sirari nchini Kenya na Tanzania malori yamepaki zaidi ya siku tisa.

Amesema malori hayo mengine yamebeba mizigo ijayoharibika kama machungwa na kwamba watu wanapata hasara kubwa.

Heche aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter huku akisema kuna haja ya mamlaka itafute namna ya mizigo kuhamishwa hata kwenye magari ya Kenya.

“Lazika mamlaka itafute namna ya mizigo kuhamishwa hata kwenye magari ya Kenya ili isiharibike na kusababisha hasara kwa watu,”. Aliandika Heche

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *