Dondoo za leo: Tanzania, Kenya wayamaliza, Mrema ataka Polepole apuuzwe,Rais wa Zambia atangaza kufungua mpaka na Tanzania

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini siku ya leo.

Tatu zinazobamba leo ni pamoja na Tanzania, Kenya wayamaliza, Mrema ataka Polepole apuuzwe na mwisho ni Zambia yafungua mpaka wake na Tanzania.

Karibu;

TANZANIA , KENYA YAMEKWISHA

NCHI za Tanzania na Kenya zimeafikiana kuwa madereva watatakiwa kupimwa ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona katika nchi zao na kupewa cheti maalum kitakachowatambulisha kutokuwa na maambukizi ambacho kitakuwa halali kwa siku 14 pekee.

Baada ya siku hizo kukamilika, madereva hao watalazimika kupimwa tena wakiwa nchini Kenya au Tanzania na endapo watagundulika, watarudishwa katika nchi zao.

Soma zaidi>>>

MREMA ATAKA POLEPOLE APUUZWE

Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi (CCM), Humphrey Polepole zinatakiwa kupuuzwa.

Amesema wao kama chama hawajawahi kusema chochote kuhusiana na ugonjwa wa Corona.

“Walijifungia kusikojulikana na wamejitokeza leo kutuaminisha kwamba ugonjwa umeisha wakati hatupimwi na maabara ya taifa imefungwa na inachunguzwa. Puuzeni aliyosema tujilinde,” andika Mrema katika ukurasa wake wa Twitter.

Soma zaidi>>>

RAIS WA ZAMBIA ATANGAZA KUFUNGUA MPAKA NA TANZANIA

Rais wa Zambia, Edgar Lungu akihutubia Taifa jioni ya leo ametangaza kufungua rasmi mpaka na Tanzania na kuruhusu wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida

Rais Lungu amesema wananchi waendelee na shughuli zao huku wakifuata maoni na ushauri wa Wataalam katika kujikinga na #COVID19

Zambia ilifunga mpaka wake na Tanzania tangu Mei 11 huku Wilaya ya Nakonde ikipigwa ‘lockdown’ ikiwa ni hatua ya kutathmini njia za kuzuia maambukizi yaliyokuwa yakiongezeka kwa kasi ndani ya Nakonde

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *