Waziri Ndalichako atangaza tarehe ya kuanza mtihani kwa kidato cha sita

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, ametangaza rasmi tarehe ya kuanza kwa mitihani ya kidato cha sita Juni 29 na kukamilika Julai 16, 2020.

Waziri Prof.Joyce Ndalichako ametangaza uamuzi huo leo huku akisema  wanafunzi ambao ni wa bweni wanatakiwa kuanza kuripoti Mei 30, mwaka huu ili ifikapo Juni mosi waanze masomo yao.

Waziri ameliagiza Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kusambaza mitihani hiyo mara moja, lakini pia kuhakikikisha matokeo yanatoka kabla ya Agosti 30, mwaka huu.

Aidha, amesema Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Vyuo Vikuu amesema,tayari bodi hiyo ina fedha kiasi cha sh.bilioni 122.8 kwa ajili ya wanafunzi wenye sifa ya kupata mikopo hiyo.

Waziri amesema kwa sasa vyuo vinatakiwa kuwasilisha nyaraka hadi Mei 28, 2020 ziwe zimefika bodi ya mikopo ili itoe fedha hizo kwa wanafunzi watakapofika vyuoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *