Mrema amvaa Lowassa amuambia amerudi utumwani

Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema uongozi ni kuwa mfano kwa kuonyesha kujali maelekezo ya wataalamu wa afya.

Mrema aliandika ujumbe huo huku akiwa ameweka picha ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa katika ukurasa wake wa Twitter.

Kiongozi huyo alimuambia amshauri mkubwa kuzingatia ushauri wa wataalamu.

Mrema aliandika ujumbe unaosomeka hivi “Uongozi ni kuwa mfano, pamoja na yote angalau angeweza kutuvusha kwa kuonyesha mfano wa kujali maelekezo ya wataalamu wa afya na WHO.. But amerudi utumwani … sad.. OK amshuri mkubwa kuzingatia ushauri wa wataalamu,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *