Mdee: Kumshikilia Idris ni matumizi mabovu ya fedha za umma hiyo picha ya Rais na mimi niliipenda

Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, amesema kuendelea kumshikilia mchekeshaji Idris Sultan ni matumizi mabovu ya fedha za umma.

“Mhe @MagufuliJP kama kweli wasaidizi wako wanamshikilia @ IdrisSultan sababu ya ile picha yake.. ambayo hata mimi niliipenda, ni matumizi matumizi mabovu ya fedha za umma,”

Mdee aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter huku akiwa ameweka picha yake aliyoipiga kipindi cha zamani.

Kiongozi huyo amesema picha yake ya zamani anajivunia nayo kwa sababu ni sehemu ya historia yake.

“Hako kapucha ka ebzi hizo nilikuwa mlugaluga/ kauzu sana… Lakini najivunia nako sababu ni sehemu ya historia yangu,” aliandika Mdee katika ukurasa wake wa Twitter.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *