Dondoo za leo: Lema asema wanafanya mchezo kwenye Corona, Mrema amvaa Lowassa amuambia amerudi utumwani na Mdee asema kumshikilia Idris ni matumizi mabovu ya fedha za umma

 

Habari ya asubuhi mdau wetu wa Opera News, matumaini yetu umeamka salama.

Karibu kwenye dawati letu la Dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazobamba asubuhi ya leo MeiĀ  22, 2020.

Habari hizo ni Mbunge wa Arusha mjini (Chadema) amesema wanafanya mchezo kwente ugonjwa wa Corona na kwamba utaleta majuto makubwa kulikoni?, mrema amvaa Lowassa amemuambia amerudi kundini na Mdee ameeleza kushikiliwa kwa Idris ni matumizi mabovu ya fedha za umma kwani hata yeye aliipenda hiyo picha.

Karibu msomaji wetu;

LEMA ASEMA WANAFANYA MCHEZO KWENYE CORONA ITALETA MAJUTO MAKUBWA

Mbunge wa Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema, amesema wanafanya mchezo kwenye ugonjwa wa Corona hali ambayo imesababisha wananchi kuishi maisha ya kawaida.

“Mmefanya watu wanaishi maisha ya kawaida sana mitaani kwa sasa. Ni jambo baya kubashiri majanga kwa nchi yako,” amesema Lema.

Soma zaidi

MREMA AMVAA LOWASSA AMUAMBIA AMETUDIA UTUMWANI

Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema uongozi ni kuwa mfano kwa kuonyesha kujali maelekezo ya wataalamu wa afya.

Mrema aliandika ujumbe huo huku akiwa ameweka picha ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa katika ukurasa wake wa Twitter.

Kiongozi huyo alimuambia amshauri mkubwa kuzingatia ushauri wa wataalamu.

Soma zaidi

MDEE: KUMSHIKILIA IDRIS NI MATUMIZI MABOVU YA FEDHA ZA UMMA

Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, amesema kuendelea kumshikilia mchekeshaji Idris Sultan ni matumizi mabovu ya fedha za umma.

“Mhe @MagufuliJP kama kweli wasaidizi wako wanamshikilia @ IdrisSultan sababu ya ile picha yake.. ambayo hata mimi niliipenda, ni matumizi matumizi mabovu ya fedha za umma,”.

Soma zaidi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *