Askari aliyeokoa uhai wa mtoto wa mwaka mmoja aliyetupwa chooni apandishwa cheo

Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga amempandisha cheo Danis Minja wa jeshi hilo kwa ujarili wake wa kuingia kwenye shimo la choo na kufanikiwa kumuokoa mtoto mwenye umri wa mwaka moja na nusu katika Kata ya Murgwanza wilaya ya Ngara mkoani Kagera.

Askari huyo wa kikosi cha Zimamoto na uokoaji amepandishwa cheo kutoka Constable na kuwa Koplo.

Video ambayo inaonyesha jinsi alivyomuokoa mtoto huyo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Baadhi wa watu waliyoiona video hiyo walimsifu askari huyo kwa ujasiri aliouonyesha huku wenginine wakisema anastahili kuongezewa cheo kwa jinsi alivyojitolea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *