Zitto Amshukia Rais Magufuli “Ameamua Kwenda Tu Kama Gari Bovu”


Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe amesema Rais John Magufuli amepoteza muelekeo kwenye vita dhidi ya virusi vya Corona nchini na anakwenda kama gari bovu

Katika ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake rasmi wa Twitter Zitto amesema Rais haamini tena kwenye Sayansi kama ilivyo kwa nchi zingine

“Rais Magufuli ambaye kitaaluma ni Mkemia, japo aliwahi kushiriki kikombe cha babu, haamini tena kwenye sayansi. Ameamua tujiendee tu kama gari bovu, hata wasaidizi wake wanaunga mkono mwelekeo wake wa “kuachana kabisa na utaratibu wa kupima” ameandika Zitto

Ujumbe wa Zitto unakuja saa chache baada ya Rais John Magufuli kutangaza kufunguliwa kwa vyuo vikuu nchini kiwa ni baada ya kupungua kwa kiasi kikubwa kwa wagonjwa wa  COVID-19 nchini

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *