WHO Kufanyia Majaribio Dawa Ya Corona Ya Madagascar


Katibu mkuu wa Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia Afya (WHO) Tedros Ghebreyesus amesema shirika hilo linaangalia uwezekano wa kushirikiana na Madagascar juu ya dawa yake ya kutibu virusi vya Corona

Katika Ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wa Twitter amesema kulingana na mwenendo wa kupungua kwa wagonjwa wa Corona nchini humo WHO inatazamia kuangalia njia zilizotumika kupunguza wagonjwa hao ikiwemo Dawa iliyogunduliwa nchini humo

“Nimefanya mazungumzo na rais wa Madagasca tumeshauriana juu ya kufanya uchunguzi wa kitabibu nchini humo baada ya kupungua kwa idadi ya wagonjwa na tumekubaliana umoja ndio mbinu itayotusaidia kuvuka tatizo hili” ameandika

Dawa ya miti shamba iliyogunduliwa nchini humo tayari imeshaanza kusambazwa kwenye mataifa kadhaa ya Afrika ikiwemo Tanzania, Niger, Liberia na Guinea Bissau

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *