Waziri Ummy : Tulipanga Kuweka Vitanda 1000 Uwanjani Kutibu Corona


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameweka wazi kuwa serikali ilipanga kuweka vitanda zaidi ya 1000 kwenye uwanja wa sabasaba kwa ajili ya kuwatibu wagonjwa wa Corona kutokana na kujaa kwa wagonjwa hao kwenye vituo vilivyotengwa kutolea huduma

Ummy amenukuliwa na mtandao swahili times amesema mpango huo umefutwa kutokana na wagonjwa kupungua nchini hivyo waliobaki ni waliopo hospitali tu na wanaendelea vizuri na matibabu

“Tulikuwa tumeandaa Uwanja wa Sabasaba kwa ajili ya kuweka vitanda 1,000 vya wagonjwa wa corona, lakini tumerudisha uwanja kwa sababu wagonjwa wamepungua, na waliobaki wapo hospitalini.” Amenukuliwa

Mapema leo Rais John Magufuli ameagiza kufunguliwa kwa baadhi ya huduma za kijamii (Vyuo na Kurejesha michezo) kutokana na kupungua kwa kiaisi kikubwa kwa wagonjwa wa Covid19 nchini

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *