Waziri Mwalimu amshukuru Rais Magufuli kwa kumtia moyo

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amemshukuru Rais John Magufuli kwa kuendelea kumuamini na kumtia moyo katika kusimamia sekta ya Afya nchini.

“Asante Mhe Rais Dk @ Magufuli JP kwa kuendelea kuniamini na kunitia moyo katika kusimamia sekta ya Afya nchini hasa katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya # Covid19,” Mwalimu aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter

Aliongezea “Naahidi kuitumikia nchi yangu kwa bidii, uaminifu na maarifa zaidi,”

Leo Rais Magufuli alimpongeza Waziri Mwalimu huku akikuambia anajua alimtesa sana kwani alikuwa akimpigia simu zaidi ya mara nane.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *