Denmark Yafuata Njia Za JPM, Kufungua Shule,Vyuo Na Mipaka


Ikiwa ni saa kadhaaa baada ya serikali ya Tanzania kufungua vyuo vikuu uamuzi huo pia unaweza kuchukuliwa na Serikali ya Denmark mara bbada ya kutangaza kuanza kulegeza masharti yaliyowekwa kudhibiti maambukizi ya covid nchini humo kwa kuwaza kufungua Shule na mipaka yake

Denmark inaingia hatua ya pili ya kufungua nchi ambapo maeneo ya tamaduni kama vile makumbusho, sehemu za kuonesha filamu na bustani za wanyamapori zitafunguliwa kuanzia Juni 08 mwaka huu

Hata hivyo, Serikali imesema ili kupunguza hatari ya maambukizi mapya, sehemu ambazo zinaonekana ni hatarishi ikiwemo kumbi za starehe na maeneo ya kuogelea yataendelea kufungwa

Denmark imerekodi visa 11,128 na wagonjwa 9,536 wamepona. Vifo 554 vimeripotiwa nchini humo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *