Wema amkumbuka Kanumba kwa kuposti picha tano, za kazi, mahaba na bata

Red Valentine Part 1 - Steven Kanumba, Wema Sepetu (Official Bongo ...

Nyota wa Bongo Movie Wema Sepetu ameomboleza kifo cha msanii mwenzake na mpezi wake wa zamani Steven Kanumba kwa kuposti picha tano akiwa naye katika matukio tofauti.

Miongoni mwa picha zilizopostiwa na Wema zile zambazo walikuwa naye maeneo ya starehe, katika kazi na wakati wa mahaba.

Pamoja na kuposti picha hizo Wema aliamtakia pumziko jema kipenzi chake huku akimwambia kuwa amemkumbuka na atakuwa katika moyo wake muda wote.

“In our Hearts Always & Forever. Picha ya Kwanza- Kwa mara ya Kwanza Booboo wangu amepata award yake ya Kwanza ya John Reeber. Picha ya pili- Moja katika scenes za movie yetu ya kwanza pamoja “A point of no return”

“Picha ya tatu- moja kati ya scenes za movie ya Pili “Red Valentine”

Picha ya nne- tulikuwa Kwenye Band Akudo Impact… Booboo alipenda sana Mziki wa Band… We used to have a good time… Picha ya Tatu- Mapenzi Tele… Ona macho yetu…Tulikuwa sooo inlove… “I miss you so much… Loving u all day, eerday booboo.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *