Ungezaa Mzungu Wasingekufukuza- Tanasha Alaumiwa kujifungua Mtoto Anayefanana na Mondi

Tanasha Donna taps into spiritual realm after split ...

Tanasha Donna alitengana na Diamond miezi miwili iliyopita baada ya uhusiano wao kugonga mwamba

Wawili hao walijaliwa mtoto wa kiume pamoja

Shabiki mmoja amejitokeza kudai kuwa mtoto huyo ndiye chanzo cha kutengana kwa wawili hao

Mwanao Diamond Platnamz na Tanasha Donna anazidi kukua kwa kasi mno, picha yake iliyopachikwa katika mtandao wa Instagram na Tanasha ikiwa thibitiso tosha.

Tangu wawili hao kutengana, Donna ameonekana kusonga mbele na maisha yake pasi kujali Mondi hivi majuzi akijitokeza na kutangaza kuhusu jengo jipya la kifahari alilojinunulia.

Hayo kando, kuthibitisha kuwa amekuwa mzazi na mlezi wa kuweza kuigwa, Donna aliipachika picha ya mwanawe katika ukurasa wake wa Istagram, katika picha hiyo alikuwa ameifunika sura ya mtoto huyo.

Wengi mashabiki wake walijitokeza kumrundia sifa kwa kuwa mlezi shupavu na mzazo bora kutokana na jinsi alivyomtunza mtoto huyo licha ya kutokuwepo babake.

Huku wengi wakimsifia, mmoja ambaye alikuwa na maoni tofauti alijaribu kumkumbusha kuhusu chanzo cha kusambaratika kwa uhusiano wake na Diamond.

Kulingana na shabiki huyo aliyetabulika kama afs19680, mtoto wake ndiye alikuwa chanzo cha kuvunjika kwa uhusiano wao. Alidai kuwa Donna angelijifungua mtoto mzungu, hangelifukuzwa na Mondi.

‘‘Ungezaa mzungu wasinge kufukuza’’, afs19680 aliandika.

Lakini swali ni je, Donna angewezaje kujifungua mtoto mzungu ikiwa Mondi ambaye ni baba wa mtoto huyo si mzungu, ama alipaswa kutumia njia gani ili kujifungua mtoto mzungu?

Tanasha's spiritual post that has left many questioning Diamond ...

Diamond kwa upande wake hajafunguka kuhusu chanzo cha kutengana na kipusa huyo wala kukisia kuwa mtoto huyo ndiye chanzo cha kusambaratika kwa uhusiano wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *