Mchungaji Akiri Kuhusika Katika Wizi wa Mabavu Baada ya Kuvamiwa na Umma

Kisumu pastor arrested for involvement in robberies

Charles Odhiambo wa kanisa la Green Yellow Cross. Picha: TUKO.

Mchungaji huyo aliyetambulika kama Charles Odhiambo wa kanisa la Green Yellow Cross alikamatwa na umma wenye mori kabla kumwasilisha kwa maafisa wa polisi

Odhiambo alikiri kuhusika katika wizi akishirikiana na watawu wengine, mmoja akiwa afisa wa polisi

Polisi wamefanikiwa kuwanasa wengine wawili huku wakianza msako dhidi ya afisa huyo mmoja.

Maafisa wa polisi mjini Kisumu, Kenya wamemkamata mchungaji aliyehusika katika wizi wa mabavu akishirikiana na wengine watatu kwa kudai kuwa maafisa wa polisi.

Police bail time limit for suspects could be trebled - BBC News

Maafisa wa polisi wameanza msako dhidi ya afisa aliyetajwa kuhusika katika wizi huo. Picha; Hisani

Mchungaji huyo aliyetambulika kama Charles Odhiambo alivamiwa na umma wenye mori waliompa adabu kwa kwa makonde kabla kumwasilisha kwa polisi.

Odhiambo alikiri kuhusika katika wizi akishirikiana na wengine akiwemo afisa wa polisi anayehudumu katika kituo cha Maseno.

Inadaiwa kuwa wanne hao wamekuwa wakitumia gari aina ya Subari huku wakijidai kuwa maafisa wa polisi kabla kuwaibia wananachi.

Katika kisa kimoja, watatu hao walimuibia mwanabiashara mmoja wa Mpesa Ijumaa, Aprili 3 watu wakiwa mbioni kufunga biashara zao ili kufika majumbani mapema kulingana na agizo la serikali.

Kisumu pastor arrested for involvement in robberies

Hadi sasa maafisa wa polisi wamefanikiwa kuwakamata wengine wawili huku wakianza msako mkali dhidi ya afisa huyo wa polisi ambaye alitoweka. Walionaswa wakizuiliwa katika kituo cha polisi cha Kondele

Visa vya wizi vimeonekana kuongezeka haswa kufuatia kafyu iliyotangazwa rasmi na serikali, wezi wakichukua nafasi hiyo ya kuwaibia wananchi na biashara zao wakati wamefunga na kuelekea majumbani mapema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *