Dondoo za leo: Waziri Ummy asema hakuna mgonjwa wa ndani wa Corona hadi sasa, asakwa kwa kutupa pacha shimo la choo na wahamiaji sita na madereva watatu wanasuruka kuuliwa

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News tunatumai uko salama.

Karibu kwenye dawati letu la Dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazobamba nchini asubuhi ya leo Machi 27, 2020.

Habari hizo ni waziri wa Afya Maendekeo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema hakuna mgonjwa wa ndani wa Corona hadi sasa kulikoni? Vipi kuhusiana na mtoto wa Mbowe anayeumwa Corona? ambaye hakusafiri nje ya nchi soma habari hii kwa kina, asakwa kwa kutupa pacha shimo la choo na wahamiaji sita na madereva watatu wanusurika kuuliwa.

Karibu usome habari hizo;

WAZIRI UMMY HAKUNA MGONJWA WA NDANI WA CORONA HADI SASA

SERIKALI imesema mpaka sasa hakuna maambukizi ya ndani ya virusi vya ugonjwa wa corona, huku wagonjwa waliothibitika kuambukizwa virusi hivyo wamefi kia 13.

Pia kuanzia Januari mwaka huu mpaka sasa, wasafiri 1,890,532 wamefanyiwa uchunguzi wa ugonjwa huo, huku mpaka sasa wasafiri 245 wamewekwa karantini ya lazima kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Soma zaidi

ASAKWA KWA KUTUPA PACHA SHIMO LA CHOO

POLISI mkoani Rukwa inamsaka mama aliyejifungua watoto pacha anayedaiwa kumtupa mmoja shimo la chooni.

Mzazi huyo anayedaiwa kujifungua pacha hao siku nne zilizopita anaishi Kijiji cha Namlengwa kilichopo katika Kata ya Lyowa katika Mji Mdogo wa Matai katika Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa. Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Justine Masejo alithibitisha mkasa huo ulitokea Machi 22, mwaka huu saa 1:00 asubuhi.

Soma zaidi

WAHAMIAJI SITA NA MADEREVA WATATU WAMENUSURIKA KUULIWA

WAHAMIAJI haramu sita na madereva wa bodaboda watatu wamenusurika kuuawa na wananchi wa Kijiji cha Ibungu wilayani Ileje mkoani Songwe, baada ya kunasa kwenye mtego uliowekwa na wananchi hao.

Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo lililotokea Machi 25, mwaka huu, majira ya alfajiri kijijini hapo ni uvumi ulionea wa kuwepo watu wanaojihusisha na unyonyaji damu.

Baada ya taarifa hizo za kuonekana watu wanaodhaniwa ni wanyonya damu wakisafiri kwa kutumia pikipiki, inadaiwa wakazi hao waliweka kizuizi katika barabara kwa kupanga magogo jambo lililofanikisha kuwanasa.

Soma zaidi

Kumalizia dondoo, tuangazie dondoo muhimu kwa wagonjwa wa Kisukari

ImageKama una ndugu anaishi na kisukari, tafadhali mpe dondoo hii “Muda mzuri wa kujaribu na kununua VIATU ni jioni sio asubuhi” Kwanini?

Dk. Norman Jonas, anaeleza sababu ya kufanya hivo kuwa ni miguu huwa mikubwa wakati wa jioni kuliko asubuhi hivyo ataepuka kununua viatu vinavyombana na kumsababishia vidonda ambavyo huleta matatizo mengi.

Ni hayo tu kwa leo mdau wetu, usisahau kuacha maoni yako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *