Uongozi wa Harmonize wafunguka Album ya Afro East kupotezwa mtandaoni

Image result for harmonizeMeneja wa masanii Hamonize (Kondeboy) umezungumzia suala la albamu ya msanii huyo iliyotolewa hivi karibuni (Afro East) kuondolewa katika mitandao ya kijamii kwasababu zinazoelezwa kuwa ni masuala ya hati miliki.

Masaa kadhaa yaliyopita nyimbo za msanii huyo zilishushwa katika majukwaa mbalimbali ya kimtandao lakini asubuhi ya leoMachi 26, 2020 Kondeboy amesema sasa zinapatikana katika baadhi ya majukwaa.

Baada ya tukio hilo Meneja wa Kondeboy Mjerumani amesema kuna mazungumzo na youtube pamoja na wadau wengine ambao nyimbo zao zimeshushwa na mambo yanakwenda vizuri.

Amesema baadaye baada kumaliza changamoto iliyopo wataeleza kilichotokea “Albamu yetu imerudi katika baadhi ya majukwaa na baadaye tutaweza kuzungumza”

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *