Unyunyuziaji wa dawa za kupambana na Corona Dar wazua mjadala

Zoezi la unyunyuziaji wa dawa za kuua virusi vya corona limeanza katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam ambapo wanaofanya kazi hiyo hupita mitaani na kunyunyuza.

Upulizaji huo umeanzia katika Manispaa ya Kinondoni ambapo wapulizia wa dawa ya kuua vijidudu walipita maeneo ambayo mara nyingi huwa na mkusanyiko ya watu na kupuliza dawa hiyo.

Hata hivyo baada ya watu hao kuonekana wakipuliza dawa hiyo mjadala uliibuka mitandano watu wakishangaa ni vipi virusi viuliwe na dawa ya kuua wadudu na wengine walihoji kwanini mashine moja ihhudumie eneo kubwa tofauti na ilivyofanyika China ambapo eneo kubwa lilipulizwa dawa kwa wakati mmoja.

Vilevile wapo waliopongeza mpango huo wakisema unaonyesha hatua mudhubuti na nia ya Serikali kukabiliana na mlipuko wa virusi hivyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *