Serikali imesema wagonjwa wa Corona wapo 13 na waliowekwa karantini kwa uchunguzi ni 245

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema jumla ya wagonjwa 13 wana Corona na watu 245 wamewekwa karantini kuchunguzwa zaidi.

“Sampuli 273 zilichunguzwa na kubainika watu13 wamekutwa na corona ambao wanatoka Arusha ni wawili, Dar es Salaam nane, Kagera mmoja na Zanzibar wawili.
Kati ya wagonjwa 13 ni mmoja ataruhusiwa,” amesema

Mwalimu amesema raia ni nane na raia wa kigeni ni watano.

“Naomba nitoe ufafanuzi kwa mgonjwa wa Kagera ni dereva wa malori anaenda DRC na Tanzania hivyo ugonjwa huo amekuja nao,” amesema.

“Mgonjwa wetu wa kwanza amepona tumempima sampuli mara tatu hakuna Corona kwa sasa tunamruhusu kwenda nyumbani. Isabella amepona anatakiwa kupokelewa na jamii,” amesema.

Amesema kwa sasa wanachokifanya ni kutoa elimu ya wananchi kuacha kuwanyanyapaa wagonjwa wa Corona.

Waziri Mwalimu amesena tangu Machi 23 mwaka huu wasafiri 111 waliotoka nchi zilizoathirika na wagonjwa wametengwa kwa ajili ya uchunguzi wa Corona na
Zanzibar 134 wamewekwa kwenywe karantini.

Aidha, amewataka Wakuu wa mikoa kuhakikisha wanawaweka watu karantini kwenye maeneo ambayo watamudu hizo gharama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *