Rais Magufuli: Mkajifungie mahala na kuifanyia kazi hii ripoti kuna changamoto nyingi zimejitokeza

Rais John Magufuli amewataka viongozi wa serikali kujifungia na kuijadili kwa kina ripoti iliyowasilishwa leo kwani inachangamoto nyingi.

Rais Magufuli amesema katika ripoti iliyowasilishwa leo na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabbu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuna changanoto nyingi ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi.

“Sitaki kuyarudia imetajwa Tamisemi, yametajwa wizara mbalimbali kuna miradi mingine imewasilishwa bila nyaraka tuanze kuyafanyia kazi na tuipeleka hii ripoti bungeni ikafanyiwe kazi na tutoe majibu maana hili ni bunge la mwisho yasiwe vipotoro kwa watendaji wapya mwakani,”.

Aliongezea kuwa “Ikiwezekana tujifungie mahali tufanyie kazi na hili naona nikuachie Waziri Mkuu ulibebe na watendaji wako, mawaziri wako, makatibu wakuu hatujazuiliwa kukutana,” alisema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *