Rais Magufuli: Kuna wengine wanadhani tutaahirisha uchaguzi nani anayetaka kukaa katika haya maofisi muda wote?

Rais John Magufuli amesema licha ya kuwepo kwa ugonjwa wa Corona uchaguzi utafanyika.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo wakati akipokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ya mwaka 2018/19 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dosoma

“Kazi lazima ifanyike kuna wengine wanazani tutaahirisha uchaguzi nani anayetaka kukaa katika haya maofisi muda wote,”

Rais Magufuli amesema hawajazuia kufanya mikutano ya kawaida hata nchi zilizoathirika na Corona zinafanya vikao.

“Hatujazuiliwa kukatana leo ninasoma gazeti moja linasema madiwani wafanya kikao cha madiwani sijui alizani vikao vya madiwani vimezuiliwa kwa sababu ya Corona sisi tunaendeelea kukutana n ahata bunge linaendelea n ahata nchi zilizoathirika na ugonjwa huo bado mabunge yao hayajafungwa, mabaraza yao hayafungwa na wanaendelea na kazi,” amesema Rais Magufuli

Aliongezea kuwa “Inaonyesha mwandishi bado hajaelewa vizuri maana ya dhana hii kazi lazima iendelee kufanyika na uchaguzi tutafanya ,” mesema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *