Rais Magufuli amtumbua Balozi wa Ethiopia kwa ubadhirifu

Rais John Maguli amesema balozi wa Tanzania nchini Ethiopia tayari ameshamrudisha nchini kutokana na ubadhlifu ambao ulifanyika wa matumizi mabaya ya fedha za umma.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo wakati akipokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ya waka 2018/19 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Amesema katika ripoti iliyowasilishwa imeonyesha ubadhilifu katika balozi za Tanzania na tayari amemrudisha nchini balozi huyo.

“Mmetusaidia Takukuru kwa ripoti yenu kuhusu wizi wa  mabilioni uliofanywa  na  balozi wetu wa Ethiopia,”amesema Rais

Aliongezea kuwa: “Balozi wa Ethiopia nimeshamrudisha sio balozi tena…na hii itakuwa ni fundisho kwetu sisi kwamba ukiharibu kwenye sehemu yako ujiandae kubeba msalaba,” amesema Magufuli

Aidha, amewaomba viongozi kuhakikisha hiyo ripoti iwasaidia kurekebisha yale ambayo yametajwa ili kuyaboresha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *