Nyalandu asisitiza hatua madhubuti kwa nchi masikini kukabiliana na Corona

Wanasiasa nchini hususani wa upinzani wameendelea kusisitiza juu ya kuchukuliwa kwa hatua madhubuti hapa nchini katika kukabiliana na virusi vya Corona.

Mpaka sasa nchini Tanzania visa 13 vimeripotiwa na mpaka sasa hakuna kifo kilichotokea waathirika bado wanaendelea na uangalizi wa kitabibu.

Kupitia ukurasa wa Twitter kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amenukuu taarifa ya Jarida la uchumi la Economist akisema Virusi hivyo vitazivuruga zaidi nchini Masikini.

Baada ya posti hiyo Mwenyekiti wa Chadema kanda ya kati Lazaro Nyalandu amesema tishio ni halisi na hatua maudhubuti zinapaswa kuchukuliwa kabla ya kuchelewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *